Machafuko yaendelea kaskazini mashariki mwa Nigeria, watu 8 wauawa
Watu wanane wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika miripuko ya mabomu iliyotokea katika kambi mbili za wakimbizi, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Kundi la walinzi la wananchi limesema kuwa, watu wasiopungua 8 wameuawa baada ya wanawake waliokuwa wamejifunga mabomu kushambulia kambi mbili huko Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno,
Mji wa Maiduguri umekuwa ukikumbwa na mashambulizi ya kujilipua kwa mabomu yanayofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi na na kiwahabi la Boko Haram na akthari ya watu wanaohusika na mashambulizi hayo ni wanawake.
Kwa karibu miaka minane iliyopita Nigeria imekuwa uwanja wa mashambulizi ya kigaidi ya kundi la Bko Haram ambayo yanawalenga askari na raia wa kawaida. Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianzisha hujuma zake mwaka 2009 na hadi sasa karibu watu elfu 20 wameuawa na zaidi ya milioni mbili kujeruhiwa.
Mbali na wimbi la mashambulizi ya kigaidi, Nigeria pia inakabiliwa na migogoro ya ardhi na pia makundi yanayotaka kujitenga ambayo yamekuwa yalivuruga usalama na amani ndani ya nchi hiyi ya magharibi mwa Afrika.