Watu zaidi ya 100 watiwa mbaroni Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32606-watu_zaidi_ya_100_watiwa_mbaroni_kongo
Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limeripoti kuwa watu zaidi ya mia moja wametiwa mbaroni katika maandamano ya amani yaliyofanyika juzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupinga hatua ya Rais Joseph Kabila ya kusalia madarakani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 02, 2017 14:25 UTC
  • Watu zaidi ya 100 watiwa mbaroni Kongo

Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limeripoti kuwa watu zaidi ya mia moja wametiwa mbaroni katika maandamano ya amani yaliyofanyika juzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupinga hatua ya Rais Joseph Kabila ya kusalia madarakani.

Mtafiti wa Amnesty International nchini humo ameeleza kusikitishwa na hatua ya polisi wa Kongo ya kutumia mabavu na silaha za kivita dhidi ya wananchi wanaoandamana na kueleza kuwa, watu wanne walijeruhiwa pia mbali na kutiwa mbaroni wengine 100 katika maandamano hayo ya amani yaliyofanywa juzi Jumatatu kote nchini Kongo.  

Mtafiti huo wa Shirika la Msamaha Duniani nchini Kongo ametaka kuachiwa huru haraka na bila ya masharti watu wote waliotiwa nguvuni katika maandamano ya amani ya juzi wakiwemo waandishi habari. Taarifa zilizokusanywa na shirika hilo zimeeleza kuwa, askari usalama wa Kongo walitumia gesi ya kutoa machozi na silaha za kivita dhidi ya waandamanaji katika miji sita ya nchi hiyo. Maandamano hayo ya amani yalifanyika katika miji 11 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  

Maandamano ya amani ya wananchi katika mji mkuu Kinshasa