Mar 18, 2016 03:06 UTC
  • Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya Boko Haram misikitini Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi dhidi ya misikiti mmoja yanayofanywa na na genge la kitakfiri la Boko Haram nchini Nigeria.

Mbali na kulaani shambulio hilo, Ban Ki-moon amelaani pia shambulizi la hivi karibuni lililowalenga Waislamu waliokuwa wanasali katika msikiti mmoja kwenye viunga vya mji wa Maiduguri ambapo Waislamu 22 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, mbali na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo, Ban ameitaka serikali ya Nigeria kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatia mbaroni wahusika wa jinai hiyo. Itafahamika kuwa, Jumanne iliyopita wanawake wawili waliokuwa wamevaa nguo za kiume walishambulia Waislamu waliokuwa wanasali sala ya Alfajiri msikitini katika eneo la Mulai mjini Maiduguru katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Hili ni shambulio la pili - kwa mwezi huu wa Machi - kufanywa na kundi hilo la kigaidi ambalo lilitangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Tags