Watu 19 wametekwa nyara kusini mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34071-watu_19_wametekwa_nyara_kusini_mwa_nigeria
Polisi ya Nigeria imesema kuwa, watu 19 waliokuwa ndani ya basi wameshambuliwa na kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha huko katika Bandari ya Harcourt kusini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 08, 2017 12:13 UTC
  • Watu 19 wametekwa nyara kusini mwa Nigeria

Polisi ya Nigeria imesema kuwa, watu 19 waliokuwa ndani ya basi wameshambuliwa na kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha huko katika Bandari ya Harcourt kusini mwa nchi hiyo.

Polisi ya Nigeria imetangaza leo kuwa shambulio hilo lilifanywa jana Alhamisi na kwamba hadi sasa wamefanikiwa kuwanusuru watu 12 kutoka mikononi mwa watekaji nyara. Hilo ni shambulio la pili kuwahi kufanywa na watekaji nyara katika wiki mbili za hivi karibuni katika Bandari ya Harcourt. 

Magenge ya watekaji nyara katika bandari ya Harcourt kusini mwa Nigeria 

Tarehe 28 mwezi Agosti uliopita pia watu waliokuwa na silaha waliwateka nyara abiria 16 waliokuwa ndani ya basi moja katika bandari hiyo hiyo.

Vitendo vya utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidia vimeenea katika eneo tajiri kwa mafuta huko kusini mwa Nigeria kiasi kwamba, magenge ya watu wenye silaha  yamekuwa yakiwashambulia wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya mafuta na ya yale ya kigeni yanayoendesha shughuli zao katika eneo hilo.