Wakuu wa Ulinzi Afrika Mashariki wakutana Uganda
(last modified Tue, 21 Nov 2017 02:40:21 GMT )
Nov 21, 2017 02:40 UTC
  • Wakuu wa Ulinzi Afrika Mashariki wakutana Uganda

Wataalamu wa masuala ya ulinzi kutoka nchi za Afrika Mashariki wanakutana nchini Uganda kujadili njia za kuimarisha amani na usalama kieneo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya uUinzi ya Uganda imesema, mkutano huo wa siku tano ulioanza jana Jumatatu utajadili Itifaki ya Amani na Usalama katika eneo la Afrika Mashariki. Aidha, taarifa hiyo imesema, mawaziri wa ulinzi wa kanda hiyo watakutana Ijumaa wiki hii baada ya mikutano ya kiufundi kumalizika.

Nchi za Afrika Mashariki zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Bendera za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Januari mwaka 2014 Uganda, Kenya na Rwanda zilitia saini mkataba wa kuanzisha Ulinzi, Amani na Usalama wa Pamoja.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, nchi hizo tatu zitaunda ardhi ya pamoja ya ulinzi na hilo linamaanisha kuwa nchi moja ikivamiwa inahesabiwa ni hujuma dhidi ya nchi zote tatu.

Mapatano hayo pia yanawezesha nchi hizo kushirikiana katika kukabiliana na vitisho vya usalama.

Tags