UNHRC kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu S. Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3700-unhrc_kuchunguza_ukiukwaji_wa_haki_za_binadamu_s._kusini
Umoja wa Mataifa utaanza kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 24, 2016 03:45 UTC
  • UNHRC kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu S. Kusini

Umoja wa Mataifa utaanza kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) limetangaza kwamba, limeunda kamati ya wanachama watatu ambao watachunguza ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi ya Sudan Kusini. Awali baraza hilo lilikuwa likichunguza suala la kutumwa mtaalamu mmoja nchini Sudan Kusini kwa ajili ya kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo, lakini wanachama wa Umoja wa Mataifa wamechukua uamuzi wa kuundwa kamati ya watu watatu itakayochunguza suala hilo katika kipindi cha mwaka mmoja.

Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kwamba, itashirikiana na kamati hiyo ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa. Kamati hiyo itachunguza ukiukaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na ubakaji unaofanywa na makundi ya watu, kuharibiwa vijiji na mashambulizi yanayofanywa dhidi ya raia ambayo yanaweza kutambuliwa kuwa ni jinai za kivita.

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi katika machafuko ya ndani Sudan Kusini.