Waziri wa Sheria wa Algeria: Waalgeria 226 wamejiunga na Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37799-waziri_wa_sheria_wa_algeria_waalgeria_226_wamejiunga_na_daesh
Waziri wa Sheria wa Algeria ametangaza kuwa raia wa nchi hiyo wasiopungua 226 wameelekea katika nchi za Iraq na Syria kwa ajili ya kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 19, 2017 04:33 UTC
  • Waziri wa Sheria wa Algeria: Waalgeria 226 wamejiunga na Daesh

Waziri wa Sheria wa Algeria ametangaza kuwa raia wa nchi hiyo wasiopungua 226 wameelekea katika nchi za Iraq na Syria kwa ajili ya kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh.

Tayeb Louh ameeleza kuwa idara ya mahakama ya Algeria imetoa kibali cha kimataifa cha kutiwa mbaroni raia hao.

Tayeb Louh, Waziri wa Sheria wa Algeria  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria pia hivi karibuni alitangaza kuwa kundi la kigaidi la Daesh limewatolea wito mamluki wake kuhamia Libya, katika eneo la ukanda wa pwani na katika nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara barani Afrika baada ya kupata pigo huko Syria na Iraq. 

Abdulqadir al Masahil aidha amezitolea wito nchi za Kiafrika kushirikiana zaidi katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh. Hali ya mgogoro ilianza huko Syria mwaka 2011 na huko Iraq tangu mwaka 2014 kufuatia hujuma kubwa ya makundi ya kigaidi chini ya uungaji mkono wa Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao ikiwemo Imarati; lengo kuu likiwa ni kubadili hali ya mlingano katika Mashariki ya Kati kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. 

Majeshi ya Syria na Iraq hivi karibuni yalifanikiwa kufunga faili la kundi la kigaidi katika nchi mbili hizo kwa kusaidiwa na washauri wa masuala ya kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.