Maveterani Zimbabwe: Jeshi kama lingechelewa kumtimua Mugabe, tungemtimua sisi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38265-maveterani_zimbabwe_jeshi_kama_lingechelewa_kumtimua_mugabe_tungemtimua_sisi
Mashujaa wa vita vya ukombozi nchini Zimbabwe wametangaza kwamba, walikuwa wamepanga mkakati wa kumuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe wiki chache kabla ya jeshi kumtimua.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 29, 2017 12:33 UTC
  • Maveterani Zimbabwe: Jeshi kama lingechelewa kumtimua Mugabe, tungemtimua sisi

Mashujaa wa vita vya ukombozi nchini Zimbabwe wametangaza kwamba, walikuwa wamepanga mkakati wa kumuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe wiki chache kabla ya jeshi kumtimua.

Maafisa wa chama cha mashujaa wameliambia gazeti binafsi la NewsDay la nchi hiyo kwamba, walikuwa wamepanga kuvamia makazi ya Mugabe Novemba mwaka huu na kumshurutisha kiongozi huyo kujiuzulu na kwamba jeshi liliingilia kati kabla ya wao kuchukua hatua hiyo hapo tarehe 15 Novemba.

Christopher Mutsvangwa, mwenyekiti wa chama cha mashujaa wa vita vya ukombozi Zimbabwe

Aidha wamesema kuwa hata Emmerson Mnangagwa, Rais wa sasa wa Zimbabwe hakujua kilichokuwa kimepangwa na maveterani hao dhidi ya Robert Mugabe. Katika hatua nyingine mashujaa hao wa vita vya ukombozi nchini Zimbabwe wamemkosoa Mnangagwa kutokana na hatua ya kuwa mwaminifu kupitiliza kwa kwa Mugabe kabla ya kutimuliwa. "Tulikuwa na tatizo na uaminifu wake kama kipofu ambao haukuthaminiwa na Mugabe.”

Rais  Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe

Christopher Mutsvangwa, mwenyekiti wa chama cha mashujaa wa vita vya ukombozi Zimbabwe (ZNLWVA) amesem, mashujaa hao walikuwa wamepanga kuchukua hatua za kisheria kutwaa jina la 'Zanu-PF’ kutoka kwa Mugabe ambaye alikuwa amepanga kukitumia kutetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu wa 2018.