Rais wa Zimbabwe abadilisha msimamo kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38575-rais_wa_zimbabwe_abadilisha_msimamo_kuhusu_serikali_ya_umoja_wa_kitaifa
Habari kutoka nchini Zimbabwe zinasema kuwa rais wa nchi hiyo amekubaliana na mpango wa kuweko serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 05, 2018 23:30 UTC
  • Rais wa Zimbabwe abadilisha msimamo kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa

Habari kutoka nchini Zimbabwe zinasema kuwa rais wa nchi hiyo amekubaliana na mpango wa kuweko serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo.

Rais Emmerson Mnangagwa jana Ijumaa alitangaza kukubaliana na mpango wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa kumshirikisha Morgan Tsvangirai, mpinzani mkubwa wa serikali ya nchi hiyo. Inadaiwa kuwa Mnangagwa amechukua hatua hiyo ili kuimarisha uungaji mkono wa wananchi kwa serikali yake.

Morgan Tsvangirai

 

Hatua hiyo imechukuliwa katika hali ambayo kabla ya hapo rais huyo wa Zimbabwe alikuwa anapinga vikali kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa na kushirikishwa wapinzani serikalini.

Tarehe 24 Novemba mwaka jana 2017, Mnangagwa alichukua urais wa Zimbabwe siku tatu baada ya kulazimishwa kujiuzulu rais wa zamani, Robert Gabriel Mugabe.

Mugabe aliongoza Zimbabwe kwa muda wa miaka 37 yaani tangu mwaka 1980 wakati nchi hiyo ilipofanikiwa kujipapatua kutoka katika makucha ya mkoloni wa Ulaya, Uingereza. Alilazimishwa kujiuzulu la jeshi la nchi hiyo tarehe 21 Novemba na nafasi yake kuchukuliwa na Emmerson Mnangagwa ambaye ana historia ndefu ya mapambano ya ukombozi nchini humo.