Wasudan waandamana kulalamikia kupanda kwa bei ya mkate
(last modified Tue, 09 Jan 2018 15:50:11 GMT )
Jan 09, 2018 15:50 UTC
  • Wasudan waandamana kulalamikia kupanda kwa bei ya mkate

Maandandamano ya raia wa Sudan ya kupinga ongezeko la bei ya mkate na machafuko baina ya raia na askari usalama yameendelea leo kwa siku ya tatu mfululizo.

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu leo wamekabiliana na askari usalama wa Sudan katika maandamano yanayoendelea kupinga ongezeko la bei ya mkate na ughali wa maisha.

Ripoti zinasema kuwa, malalamiko hayo ya nchi nzima yanapinga hatua iliyochukuliwa na serikali ya Khartoum ya kupandisha bei ya mkate na kwamba hadi sasa mwanafunzi mmoja ameuawa na wengine sita kujeruhiwa. 

Wanachama wa chama cha Kongresi nchini Sudan wamesema kuwa askari usalama wa serikali ya nchi hiyo wamemtia nguvuni mwenyekiti wa chama hicho kikubwa cha upinzani, Omar al Daqiir. 

Wasudani wanapinga kupanda kwa bei ya mkate

Maandamano hayo ya kupinga kupanda kwa bei ya mkate nchini Sudan yameshuhudiwa zaidi katikati ya jiji la Khartoum, na katika maeneo ya Ad-Damazin huko mashariki mwa Sudan, Nyala magharibi mwa nchi hiyo na Geneina lililoko kaskazini magharibi mwa Sudan.

Tags