Rais Mnangagwa: Uchaguzi wa Zimbabwe kufanyika baada ya miezi minne au mitano
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i39165-rais_mnangagwa_uchaguzi_wa_zimbabwe_kufanyika_baada_ya_miezi_minne_au_mitano
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametangaza kuwa, uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika katika kipindi cha miezi minne au mitano ijayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 19, 2018 00:57 UTC
  • Rais Mnangagwa: Uchaguzi wa Zimbabwe kufanyika baada ya miezi minne au mitano

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametangaza kuwa, uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika katika kipindi cha miezi minne au mitano ijayo.

Mnangagwa ambaye alishika wadhifa wa urais wa Zimbabwe mwezi uliopita baada ya jeshi na chama tawala Zanu-pf kumshinikiza Robert Mugabe aliyekuweko madarakani kwa muda kwa miaka 37 ajiuzulu amenukuliwa na vyombo vya habari akitangaza kwamba, nchi hiyo itaitisha uchaguzi mkuu miezi minne hadi mitano ijayo.

Rais Mnangagwa amesema kuwa, uchaguzi ujao wa Rais, Bunge na serikali za mitaa utafanyika katika mazingira huru na ya haki.

Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75 anatazamiwa kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama tawala cha ZANU-PF.

Robert Mugabe, Rais wa zamani wa Zimbabwe

Wakati huo huo, Roy Bennett, kiongozi wa upinzani aliyekuwa akiishi uhamishoni  amefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea katika jimbo la New Mexico nchini Marekani.

Ajali hiyo ya kuanguka helikopta imewahusisha pia watu wengine wanne waliokuwa wamefuatana naye akiwemo mkewe.

Roy Bennet ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 60 na alihesabiwa kuwa mmoja wa viongozi muhimu wa upinzani nchini Zimbabwe. 

Aliwahi kufungwa jela katika enzi za utawala wa Mugabe.