Umoja wa Mataifa waonyesha matumaini ya kufikiwa makubaliano ya amani Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i40445-umoja_wa_mataifa_waonyesha_matumaini_ya_kufikiwa_makubaliano_ya_amani_sudan_kusini
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Sudan Kusini ameeleza matarajio yake juu ya kufikiwa makubaliano ya amani ya kuhitimisha machafuko nchini humo katika mazungumzo yanayoendelea hivi sasa mjini Addis Abab, Ethiopia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 16, 2018 04:15 UTC
  • Umoja wa Mataifa waonyesha matumaini ya kufikiwa makubaliano ya amani Sudan Kusini

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Sudan Kusini ameeleza matarajio yake juu ya kufikiwa makubaliano ya amani ya kuhitimisha machafuko nchini humo katika mazungumzo yanayoendelea hivi sasa mjini Addis Abab, Ethiopia.

David Shearer amesema, licha ya kwamba serikali na wapinzani wa nchi hiyo wanaendelea na hujuma za hapa na pale, lakini kuna matumaini ya kuendelea vyema mazungumzo hayo ya amani nchini Ethiopia. Amesisitiza kuwa, katika mazungumzo ya Ijumaa ya leo ambayo yatahusu masuala ya usalama, katiba na serikali kuna uwezekano mkubwa kukapigwa hatua nzuri kwa ajili ya taifa hilo changa zaidi barani Afrika.

Mazungumzo kati ya serikali ya Sudan Kusini na wapinzani yalianza tarehe tano ya mwezi huu mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Makundi ya waasi Sudan Kusini

Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 baada ya miongo kadhaa ya mapigano makali ya kutaka kujitenga na Khartoum. Hata hivyo tangu mwaka 2013 nchi hiyo ilitumbukia katika hali ya mchafukoge baada ya Rais Salva Kiir Mayardit kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar kwamba alikula njama za kutaka kumpindua. Katika vurugu hizo maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo.