Winnie Mandela afariki dunia akiwa na umri wa miaka 81
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42556-winnie_mandela_afariki_dunia_akiwa_na_umri_wa_miaka_81
Winnie Mandela, mke wa zamani wa Mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini amefaniki dunia leo Jumatatu, Aprili 2, 2018 akiwa na umri wa miaka 81.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 02, 2018 18:50 UTC
  • Winnie Mandela afariki dunia akiwa na umri wa miaka 81

Winnie Mandela, mke wa zamani wa Mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini amefaniki dunia leo Jumatatu, Aprili 2, 2018 akiwa na umri wa miaka 81.

Winnie Mandela alikuwa mmoja wa wanaharakati wa mstari wa mbele wa kupambana na utawala wa kibaguzi wa makaburu wa Afrika Kusini.

Msemaji wa familia hiyo, Victor Dlamini amesema katika taarifa yake kwamba Winnie Mandela amefariki dunia katika hospitali moja mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Winnie ambaye alikuwa mke wa Nelson Mandela kwa muda wa miaka 38 alitoa mchango mkubwa katika mapambano ya kumaliza utawala wa makaburu nchini Afrika Kusini.

"Tuna huzuni kubwa kuutangazia umma kuwa Bi Winnie Madikizela-Mandela amefariki dunia katika Hospitali ya Netcare Milpark mjini Johannesburg Afrika Kusini leo Jumatatu," imesema sehemu moja ya taarifa iliyotolewa na familia yake.