Sheikh wa al-Azhar: Beitul-Muqaddas ni ardhi ya Waislamu
(last modified Sun, 22 Apr 2018 03:47:41 GMT )
Apr 22, 2018 03:47 UTC
  • Sheikh wa al-Azhar: Beitul-Muqaddas ni ardhi ya Waislamu

Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri amesema kuwa, Beitul-Muqaddas ni ardhi ya Kiislamu na daima itaendelea kuubakia kuwa ni ya Kiislamu.

Sheikh Ahmad Tayyib amesema, mji wa Beitul-Muqaddas una umuhimu maalumu na wa aina yake kwa Waislamu.

Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri amesema kuwa, madai ya Wazayuni kuhusiana na Quds katu hayakubaliki.

Aidha Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri  amebainisha kwamba, utambulisho wa Beitul-Muqaddas daima umekuwa ni utambulisho wa Kiislamu na utaendelea kubakia hivyo hivyo.

Masjidul-Aqswa inayopatikana huko Beitul-Maqaddas

Mji wa Beitul-Muqaddas ambao una kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganishika na Palestina  na ni miongoni mwa maeneo matukufu ya Kiislamu.

Mji wa Quds ambao mwaka 1967 ulikaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukiandamwa na njama za kila aina.

Itakumbukwa kuwa Disemba mwaka jana, Rais Donald Trump wa Marekani aliutangaza mji wa Quds (Jerusalem) ambao unaheshimiwa na Waislamu na Wakristo na Mayahudi, kuwa eti ni mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel, na kutaka kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda mjini humo, suala ambalo linaendelea kulaani hadi leo hii katika kila kona ya dunia.

Tags