IMF yatoa indhari kutokana na ongezeko la madeni ya nchi za Kiafrika
(last modified Wed, 09 May 2018 02:58:32 GMT )
May 09, 2018 02:58 UTC
  • IMF yatoa indhari kutokana na ongezeko la madeni ya nchi za Kiafrika

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umetahadharisha kuwa licha ya kuwepo ukuaji wa uchumi katika nchi za Afrika lakini madeni yanayozikabili nchi za bara hilo pia yanaongezeka.

Taasisi hiyo ya fedha ya kimataifa imetoa indhari hiyo leo na kusisitiza kuwa pamoja na kushuhudiwa ukuaji wa uchumi katika nchi za Afrika za eneo la chini ya Jangwa la Sahara, lakini nchi hizo zinakabiliwa na hatari ya kuelemewa na mzigo wa madeni kutokana kuchukua mikopo mingi sambamba na kukabiliwa na nakisi za bajeti.

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa umetangaza kuwa karibu asilimia 40 ya nchi za eneo hilo zenye pato dogo zimetanzwa na matatizo yanayohusiana na mzigo wa madeni zilionao.

Taasisi hiyo muhimu ya kimataifa ya fedha yenye makao yake mjini Washington, Marekani imeongeza kuwa nchi za Kiafrika zinahitaji uwekezaji wa kiwango cha juu cha fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu yao na kuwa na ustawi wa kijamii, lakini wakati huohuo zinapaswa zipiganie zaidi kuwa na hali ya kujitegemea ili zisije zikanasa kwenye mtego wa madeni.../

 

Tags