Morocco: Zaidi ya magaidi elfu 10 wapo barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46407-morocco_zaidi_ya_magaidi_elfu_10_wapo_barani_afrika
Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco amesema kuwa, zaidi ya magaidi elfu 10 wapo barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 28, 2018 03:44 UTC
  • Morocco: Zaidi ya magaidi elfu 10 wapo barani Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco amesema kuwa, zaidi ya magaidi elfu 10 wapo barani Afrika.

Nasser Bourita, ameyasema hayo katika kikao cha kuchunguza vitisho vya kigaidi barani Afrika ambapo amesema kuwa, zaidi ya wapiganaji elfu 10 wa makundi mawili ya Daesh (ISIS) na al-Qaidah, wapo eneo la jangwa la Sahara barani Afrika na kwamba hadi sasa wapiganaji wa Daesh wamekwishafanya mashambulizi dhidi ya nchi kadhaa za bara hilo. Nasser Bourita ameongeza kwamba, magaidi wanatumia vibaya matatizo ya nchi za Afrika na kwamba idadi ya wahanga wa hujuma za kigaidi katika nchi za bara hilo inazidi idadi ya wahanga wa nchi za Ulaya. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco, karibu kamati 50 zinazojumuisha jumbe 20 kutoka bara la Afrika, zinashirikia katika kikao cha kuchunguza vitisho vya kigaidi chini ya uenyekiti wa Morocco.

Nasser Bourita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco

Inafaa kuashiria kuwa, Morocco ni moja ya nchi ambazo akthari ya raia wake ni miongoni mwa wanachama wa magenge ya kigaidi yanayofuata idilojia ya Uwahabi. Baada ya kuibuka mgogogro wa kubuniwa nchini Syria, vijana wengi wa Morocco kwa kuhadaiwa na magenge ya kigaidi walifunga safari na kwenda nchi hiyo ya Kiarabu na kuungana na magenge hayo ya kihalifu. Hata hivyo baada ya magaidi hao kushindwa vibaya na majeshi ya Iraq na Syria, walirejea nchi zao huku wengi walielekea nchi za Kiafrika.