-
Iraq yaonya dhidi ya kuibuka upya ISIS nchini Syria
Apr 14, 2025 13:06Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein ameonya kuhusu kushadidi harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika nchi jirani ya Syria, kufuatia kuanguka kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad mwishoni mwa mwaka jana.
-
Daesh: Tumehusika na shambulio la siku ya Ashura lililoua 6 Oman
Jul 17, 2024 13:17Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limekiri kuhusika na shambulizi la kigaidi lililolenga Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wamekusanyika katika msikiti mmoja nchini Oman, kwa ajili ya maombolezo ya Ashura ya kukumbuka siku ya kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (a.s).
-
Al-Khazali: Marekani haitaki kuondoka Iraq, inatumia kisingizio cha kupambana na Daesh
Nov 25, 2023 13:03Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Iraq amesema kuwa, vikosi vya majeshi ya Marekani havina nia ya kuondoka katika nchi hiyo ya Kiarabu na vinahalalisha uwepo wao kinyume cha sheria kwa kutumia kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh ambalo limekwishakufa na kutoweka.
-
Iraq yavunja mtandao wa mabaki ya ISIS mkoani Al-Anbar
Jun 06, 2023 05:32Vyombo vya usalama nchini Iraq vimefanikiwa kusambaratisha mtandao wa mabaki ya wanachama wa kundi la kigaidi la ISIS katika mkoa wa Al-Anbar, wa magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iraq: Kambi ya Marekani inayowahifadhi magaidi mashariki mwa Syria inapaswa kuvunjwa
Apr 10, 2022 11:08Afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Iraq ametoa wito wa kuvunjwa kambi ya wakimbizi inayodhibitiwa na wanamgambo wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani karibu na mpaka wa Iraq nchini Syria, akisema kambi hiyo inayohifadhi maelfu ya magaidi wa Daesh ni tishio halisi kwa nchi yake.
-
Takwa la Russia kwa ajili ya kuondoka haraka vikosi vamizi ajinabi huko Syria
Jan 29, 2022 12:16Dmitry Polyanskiy Naibu Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema katika hotuba yake katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kuwa Russia inataka kuondoka haraka iwezekanavyo vikosi vyote vamizi ajinabi ambavyo vipo kinyume cha sheria huko Syria.
-
Shamkhani: Marekani inataka kulifufua kundi la ISIS
Dec 07, 2021 14:13Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema Marekani ilighadhabishwa mno na kitendo cha kusambaratika kwa kundi la kigaidi la ISIS katika nchi za Syria na Iraq, na hivi sasa linafanya juu chini kulifufua genge hilo ili kuzusha mgogoro mpya katika eneo.
-
Kufichuliwa jinai za kivita za jeshi la Marekani nchini Syria
Nov 14, 2021 11:12Gazeti la New York Times limetoa ripoti inayoonyesha kuwa, jeshi la Marekani limetenda uhalifu wa kivita kwa kuua makumi ya wanawake na watoto katika mashambulio ya anga liliyofanya nchini Syria kwa kisingizio cha kile kinachoitwa mapambano dhidi ya kundi la DAESH (ISIS).
-
Jeshi la Nigeria laangamiza makumi ya wanamgambo kaskazini mwa nchi
Oct 19, 2021 13:31Wanamgambo 24 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram na genge hasimu Daesh huko magharibi mwa Afrika maarufu kwa jina la ISWAP wameuawa katika operesheni mbili za wanajeshi wa Nigeria, kaskazini mashariki mwa nchi.
-
UN: Kundi la Daesh lilifanya jitihada za kuangamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia
May 12, 2021 00:47Mkuu wa timu ya Umoja wa Mataifa iliyopewa jukumu la kuchunguza jinai na uhalifu uliofanywa na kundi la kiwahabi la Daesh amesema kuwa, kundi hilo la kigaidi lilifanya jitihada za kuangamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia.