Maalibino kuwania katika Uchaguzi Malawi mwaka 2019
(last modified Fri, 29 Jun 2018 03:44:03 GMT )
Jun 29, 2018 03:44 UTC
  • Maalibino kuwania katika Uchaguzi Malawi mwaka 2019

Maalbino sita wameazimia kuwania viti katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka ujao nchini Malawi. Wagombea wote sita ni wanachama wa Chama cha wenye ulemavu wa ngozi, Albino, (APAM).

Maalbino hao wanasema moja ya malengo yao katika kuwania viti ni kutetea maslahi ya jamii yao, ambayo imekuwa ikisakamwa na vitendo vya dhulma, unyanyasaji na chuki.

Mkurugenzi wa APAM Overstone Kondowe amesema nafasi katika bunge au katika moja ya halmashauri ya wilaya nchini itawawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi yao.

Katika baadhi ya nchi za Afrika, maalbino mara nyingi huuawa na viungo vyao hutumiwa kwa imani za kishirikiana kama vinaleta utajiri na bahati.

Watoto wenye ulemavu wa ngozi, Albino

Mwaka 2014, kwa mujibu wa APAM, maalbino 22 waliuawa nchini Malawi kwa jumla ya kesi 148 za ukatili zilizoorodheshwa nchini humo.

Nchi jirani ya Tanzania pia imekuwa ikishuhudia vitendo vya mauaji ya Albino lakini kufuatia hatua kali zilizhochukuliwa na serikali uhalifu huo umepungua.