Umoja wa Afrika wampongeza Mutharika kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i131250-umoja_wa_afrika_wampongeza_mutharika_kwa_kuibuka_mshindi_katika_uchaguzi_wa_urais
Umoja wa Afrika umempongeza Peter Mutharika kwa kushinda uchaguzi wa urais wa Malawi na kuwasifu wananchi wa Malawi kwa kuendesha kampeni za uchaguzi kwa amani na utulivu.
(last modified 2025-10-23T05:45:52+00:00 )
Sep 26, 2025 02:31 UTC
  • Umoja wa Afrika wampongeza Mutharika kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais

Umoja wa Afrika umempongeza Peter Mutharika kwa kushinda uchaguzi wa urais wa Malawi na kuwasifu wananchi wa Malawi kwa kuendesha kampeni za uchaguzi kwa amani na utulivu.

Mwanasiasa huyo mkongwe amechaguliwa tena kwa kuibuka na ushindi wa takriban asilimia 57 ya kura zote ili kuongoza nchi  hiyo yenye jamii ya watu milioni 21.

Mutharika, ambaye alikuwa rais wa tano wa Malawi kuanzia mwaka 2014 hadi 2020, ameshinda kwa kupata kura milioni 3 (asilimia 56.8) na kumshinda rais wa sasa Lazarus Chakwera, aliyepata kura milioni 1.77 (asilimia 33).

Tume ya Uchaguzi ya Malawi Jumatano wiki hii ilimtangaza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika wa chama cha Democratic Progressive Party (DPP) kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16.

Mahmoud Ali Youssouf Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ametuma salamu zake za pongezi kwa rais mteule Peter Mutharika aliye na umri wa miaka 85. 

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa X akiwapongeza wananchi wa Malawi kwa kushiriki kwa hamasa, amani na utaratibu katika mchakato huu wa kidemokrasia unaoaminika." 

Mutharika, anayejulikana kwa wafuasi wake kama "baba", ataapishwa kuiongoza Malawi katika muda wa kati ya siku saba na 30 tangu alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Mutharika ameahidi kuboresha uchumi wa Malawi na kuhitimisha tatizo al uhaba wa fedha za kigeni ambao umekwamisha uagizaji wa mafuta na mbolea kutoka nje.