-
Umoja wa Afrika wampongeza Mutharika kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais
Sep 26, 2025 02:31Umoja wa Afrika umempongeza Peter Mutharika kwa kushinda uchaguzi wa urais wa Malawi na kuwasifu wananchi wa Malawi kwa kuendesha kampeni za uchaguzi kwa amani na utulivu.
-
Tume ya uchaguzi Malawi yamtangaza Mutharika mshindi rasmi wa uchaguzi wa urais
Sep 25, 2025 06:41Tume ya Uchaguzi ya Malawi imemtangaza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika wa chama cha Democratic Progressive Party (DPP) mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Septemba 16.
-
Rais wa Malawi akubali kushindwa uchaguzi wa rais hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa
Sep 24, 2025 14:08Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo, akimtaja rais wa zamani Peter Mutharika kuwa "mshindi mtarajiwa".
-
Polisi Malawi yawatia mbaroni maafisa wa uchaguzi kwa madai ya udukuzi wa data
Sep 21, 2025 06:50Polisi nchini Malawi imewatia mbaroni maafisa wanane wa uchaguzi wanaotuhumiwa kujaribu kudukua matokeo ya uchaguzi wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea kufuatia ucaguzi mkuu wa Jumanne iliyopita nchini humo.
-
Wananchi wa Malawi waandamana kulalamikia uhaba mkubwa wa petroli na dizeli
Nov 25, 2024 13:31Polisi katika mji wa Lilongwe nchini Malawi leo Jumatatu wametumia gesi ya kutoa machozi kutawanya umati wa waandamanaji waliotaka kujiuzulu Waziri wa Nishati na Madini wa nchi hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta ya petroli na dizeli katika miji mbalimbali ya nchi hiyo unaoendelea kwa muda wa mwezi mmoja sasa.
-
Wanaharakati Malawi waitaka serikali isiunge mkono jinai za Israel Gaza
Oct 08, 2024 11:46Mashirika ya kiraia nchini Malawi yameiomba serikali ya Lilongwe kutazama upya msimamo wake kuhusu vita vya Israel huko Gaza "kwa sababu mtazamo na msimamo wake wa sasa ni kinyume na maadili yake ya amani na heshima kwa ubinadamu."
-
Maelfu ya wakimbizi wa Kiafrika warejea makwao baada ya kuishi Malawi kwa miongo kadhaa
Sep 23, 2024 11:43Makumi ya wakimbizi na watafuta hifadhi kutoka nchi za Kiafrika zilizoathiriwa na vita ambao walikuwa wakiishi Malawi kwa miongo kadhaa sasa wanarejea katika nchi zao kutokana na mpango wa hiari wa serikali unaotekelezwa na serikali ya Malawi pamoja na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ili kuwarejesha makwao wakimbizi.
-
Rais wa Malawi aitangaza Jumatatu kuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya maziko ya Makamu wa Rais
Jun 16, 2024 06:08Rais Lazarus Chakwera wa Malawi ameitangaza Jumatatu ya kesho ya Juni 17 kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa ili kuruhusu raia wa Malawi kuhudhuria au kufuatilia, maziko ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo Saulos Chilima aliyefariki dunia katika ajali ya ndege siku ya Jumatatu iliyopita ya Juni 10.
-
Malawi yawataka wakulima kustafidi na soko la China ili kukuza uchumi
Apr 21, 2024 07:48Mamlaka husika nchini Malawi zinawataka wakulima wa ndani kuingia katika soko la tumbaku na soya nchini China ili kukuza akiba ya fedha za kigeni nchini humo na kuimarisha uchumi.
-
Waliofariki dunia kwa Kimbunga Freddy Malawi wakaribia 700
Mar 30, 2023 02:29Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na Kimbunga Freddy nchini Malawi, ambacho kinatajwa kuwa kimbunga kilichodumu kwa muda mrefu zaidi, imeonezeka na kufikia watu 676.