Rais Mnangagwa awataka Wazimbabwe kusonga mbele baada ya machafuko ya uchaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47429-rais_mnangagwa_awataka_wazimbabwe_kusonga_mbele_baada_ya_machafuko_ya_uchaguzi
Rais Emmerson Mnangangwa wa Zimbabwe jana alisema kuwa Wazimbabwe wanapaswa kuwa kitu kimoja ili kujenga uchumi wa nchi yao na kuwenda kando kipindi cha uchaguzi. Watu sita waliuawa katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa rais huko Zimbabwe mwezi huu.
(last modified 2026-02-03T09:36:48+00:00 )
Aug 14, 2018 03:17 UTC
  • Rais Mnangagwa awataka Wazimbabwe kusonga mbele baada ya machafuko ya uchaguzi

Rais Emmerson Mnangangwa wa Zimbabwe jana alisema kuwa Wazimbabwe wanapaswa kuwa kitu kimoja ili kujenga uchumi wa nchi yao na kuwenda kando kipindi cha uchaguzi. Watu sita waliuawa katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa rais huko Zimbabwe mwezi huu.

Akihutubia taifa kwa mara ya kwanza jana tangu atangazwe mshindi katika uchaguzi wa rais uliolalamikiwa na wapinzani, Rais Mnangagwa alisema kuwa Zimbabwe imeudhihirishia ulimwengu kuwa inaweza kuendesha uchaguzi huru na wa amani. Rais wa Zimbabwe hata hivyo amekilaumu chama kikuu cha upinzani cha Mdc kuwa chanzo cha machafuko yaliyojitokeza baada ya uchaguzi.

Polis wa kutuliza ghasia wakikabiliana na wafuasi wa upinzani mjini Harare

Akihutubia taifa katika Siku ya Maadhimisho ya Mashujaa mjini Harare, Rais wa Zimbabwe alisema kuwa wakati umefika sasa wa kuweka kando muda wa uchaguzi na badala yale wananchi wakijikite katika masuala yanayohusu mustakbali wao. Weledi wa mambo wanasema kuwa ghasia zilizoibuka baada ya chama tawala cha Zanu-pf kushinda uchaguzi huo wa kitaifa na kisha jeshi kuingilia kati ili kuzima ghasia zinakumbusha kuwa jamii ya Wazimbabwe bado imegawanyika pakubwa hata baada ya uongozi wa karibu miongo minne wa Robert Mugabe.