Watu watano wauawa sokoni nchini Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4915-watu_watano_wauawa_sokoni_nchini_burundi
Watu watano wamepigwa risasi na kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumatatu usiku kufuatia hujuma iliyofanyika katika soko moja mashariki mwa Burundi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2016 11:38 UTC
  • Watu watano wauawa sokoni nchini Burundi

Watu watano wamepigwa risasi na kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumatatu usiku kufuatia hujuma iliyofanyika katika soko moja mashariki mwa Burundi.

Hujuma hiyo ilitekelezwa na waasi ambao hawakutambuliwa katika eneo la Ruyigi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Tanzania. Mkuu wa serikali ya eneo hilo, Aloys Ngenzirabona, amesema wahalifu hao walifyatua risasi kiholela kabla ya kutoroka baada ya kuwaua watu watano.

Zaidi ya watu 400 wameripotiwa kuuawa na wengine karibu laki mbili na 40 elfu wamekuwa wakimbizi tokea mwezi Aprili mwaka jana wakati Burundi ilipotumbukia kwenye machafuko yaliyotokana na Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea tena urais nchini humo.