Homa ya Manjano yaua watu 10 nchini Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49320-homa_ya_manjano_yaua_watu_10_nchini_ethiopia
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kutokana na Homa ya Manjano kusini magharibi Ethiopia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 06, 2018 04:33 UTC
  • Homa ya Manjano yaua watu 10 nchini Ethiopia

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kutokana na Homa ya Manjano kusini magharibi Ethiopia.

WHO imesema itatuma nchini humo haraka iwezekanavyo dozi ya chanjo milioni 1.45 kutoka hifadhi yake ya dharura.

Mripuko mpya wa homa hiyo umethibitishwa katika eneo la Wolaita Zone, kusini magharibi mwa nchi tokea Agosti 21 na kwamba watu 35 wanashukiwa kuambukizwa maradhi hayo hatarishi.

Ethiopia inatazamiwa kuanza kutoa chanjo ya mara kwa mara ya Homa ya Manjano kuanzia mwaka 2020, nchi anakotoka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO.

Homa ya Manjano kama Malaria, inaambukizwa kupitia mbu

Kufikia katikati ya mwaka 2016, mamia ya watu walikuwa wamefariki dunia kutokana na homa ya manjano tangu ugonjwa huo ulipuke nchini Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 2015.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa homa ya manjano vinatokea katika bara la Afrika.