Hatimaye wapinzani wafanya maandamano nchini Zimbabwe
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49859-hatimaye_wapinzani_wafanya_maandamano_nchini_zimbabwe
Maelfu ya wafuasi wa kambi ya upinzani wamefanya maandamano ya kupinga serikali mjini Harare Zimbabwe mbele ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 30, 2018 04:34 UTC
  • Hatimaye wapinzani wafanya maandamano nchini Zimbabwe

Maelfu ya wafuasi wa kambi ya upinzani wamefanya maandamano ya kupinga serikali mjini Harare Zimbabwe mbele ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, maandamano hayo yalifanyika jana Alkhamisi ambapo waandamanaji walikuwa wamebeba mapango yaliyo dhidi ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo.

Waandamanaji hao wamelalamikia udanganyifu katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo na kumtaka Rais Mnangagwa ajiuzulu na utendeke uadilifu nchini humo.

Maandamano ya wapinzani nchini Zimbabwe

 

Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe alilazimishwa kujiuzulu mwezi Novemba 2017 na nafasi yake kuchukuliwa na Mnangagwa katika uchaguzi mkuu. Baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, Mnangagwa aliahidi kuleta ustawi wa kiuchumi nchini humo.

Hata hivyo wapinzani wanasema kulifanyika udanganyifu na uchakachuaji mkubwa wa kura kwenye uchaguzi huo.

Matatizo mapya ya kiuchumi ambayo yamewasababishia matatizo makubwa ya kimaisha wananchi wa kawaida wa Zimbabwe sambamba na kuadimika sana mahitaji ya lazima ndiyo mambo yaliyozusha hasira za wananchi hao, na fursa hiyo kutumiwa na wapinzani kumshinikiza Rais Emmerson Mnangagwa ajiuzulu.