Rais wa Malawi anakabiliwa na uchaguzi mgumu; kuchuana na aliyekuwa makamu wake
Rais Peter Mutharika wa Malawi anakabiliwa na mtihani mgumu katika uchaguzi wa wiki ijayo ambao utawakutanisha pamoja wagombea kadhaa akiwemo aliyekuwa makamu wake ambaye kwa wakati mmoja alikuwa muitifaki wake ; na sasa amegeuka na kuwa mpinzani.
Makamu huyo wa Rais wa Malawi ambaye alikuwa mchungaji anamtuhumu Peter Mutharika kwa ufisadi. Mutharika ambaye ni profesa wa zamani wa sheria aliye na umri wa miaka 78 najaribu kutetea kiti cha chake cha urais kwa muhula mwingine wa pili wa miaka mitano atakaposhiriki uchaguzi wa Rais Jumanne ijayo. Siku hiyo hiyo pia wananchi wa Malawi watapiga kura kuwachagua wabunge na magavana wa serikali za mitaa.

Itakumbukwa kuwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inategemea pakubwa misaada ya nchi wafadhili na imekumbwa na ukame mkubwa mara kadhaa na kuwaathiri mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo. Katika kampeni zake za uchaguzi, Rais Mutharika alikuwa akinadi sera zake kwamba ataboresha miundombinu na kupunguza ughali wa maisha kwa watu wa Malawi. Rais wa Malawi mwaka jana alipata pigo baada ya Saulos Chilima aliyekuwa Makamu wake wa Rais kuondoka katika chama taawala cha DPP na kuunda chama kipya kwa jina la The United Transaformation Movement (UTM).