Jun 12, 2019 07:40 UTC
  • Magaidi wa Boko Haram wauwa watu 26 kaskazini mwa Cameroon

Wanajeshi wasiopungua 17 na raia tisa wameuawa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram huko Darak kaskazini mwa Cameroon.

Shambulio hilo lilitekelezwa juzi Jumatatu. Askari usalama wa Cameroon walifanikiwa kuwatia mbaroni magaidia 40 wa kundi la Boko Haram baada ya shambulio hilo. Kundi hilo mwaka 2009 lilishika silaha na kuanzisha mashambulizi na hujuma kaskazini mwa Nigeria na kisha kujipenyeza pia katika nchi jirani  za Niger, Chad, na kaskazini mwa Cameroon. Tangu wakati huo hadi sasa, kundi la kigaidi la Boko Haram limeuwa watu zaidi ya elfu 20 huko Nigeria, Cameroon, Niger na Chad, na kuwafanya wengine zaidi ya milioni mbili kuwa wakimbizi. 

Shambulio la magaidi wa kitakfiri wa Boko Haram 

Kushindwa kukabiliana na Boko Haram serikali za nchi hizo tajwa ambako kundi hilo limejiimarisha zaidi khususan nchini Nigeria kumetoa msukumo wa kushadidishwa mapambano dhidi ya kundi hilo la kigaidi na kitakfiri. 

Tags