Aug 23, 2019 07:25 UTC
  • Tayeb Louh
    Tayeb Louh

Waziri wa zamani wa Mahakama wa Algeria ametiwa mbaroni kwa tuhuma za uchochezi na kuzuia kutekelezwa uadilifu.

Shirika rasmi la habari la Algeria limeripoti kuwa, Tayeb Louh, waziri wa zamani wa mahakama katika serikali ya Abdulaziz Bouteflika iliyopinduliwa na wananchi, jana Alkhamisi alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake, kuzuia kutekelezwa uadilifu, kufanya uchochoezi na kubuni nyaraka bandia za serikali.

Tayeb Louh mwenye umri wa miaka 68 ni miongoni mwa mawaziri watiifu kwa Bouteflika ambaye tarehe pili Aprili mwaka huu alilazimishwa na wananchi kung'oka madarakani kwa nguvu. Louh alikuwemo katika serikali zote za Bouteflika kuanzia mwaka 2002 hadi 2019.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Algeria alisema mwishoni mwa mwezi Julai kuwa, ameanzisha uchunguzi kuhusu vitendo vya Tayeb Louh kama vile kufanya jinai na ufisadi wa kisiasa na kifedha.

Abdulaziz Bouteflika aliyeng'ang'ania madaraka mpaka wananchi wakamng'oa kwa nguvu madarakani

 

Katika kiindi cha miezi ya hivi karibuni, mahakama ya Algeria imeanzisha uchunguzi kuhusu ufisadi wa viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Bouteflika ambaye uongozi wake ulianza mwaka 1999 na kuhitimishwa na wananchi mwaka 2019 waliochoshwa na uongozi wake mbaya.

Mawaziri Wakuu wawili wa zamani, mawaziri wengine 9 wa zamani na mkuu mmoja wa zamani wa polisi, wakurugenzi wengi wa mashirika ya serikali na karibu wafanyabiashara 10 maarufu, ni miongoni mwa watu mashuhuri zaidi wa utawala wa Bouteflika waliotiwa mbaroni huko Algeria

 

Tags