Sep 02, 2019 07:41 UTC
  • Magaidi kadhaa wa Boko Haram wauawa kaskazini mashariki mwa Nigeria

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limeshambulia kwa ndege maficho ya magaidi wa Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kuangamiza magaidi kadhaa.

Vyombo vya habari vimenukuu taarifa ya jeshi la Nigeria iliyotolewa jana ikisema kuwa, ndege za kijeshi za nchi hiyo zimeshambulia maficho ya magaidi wa Boko Haram katika eneo la Yowe, mkoani Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuuga magaidi kadhaa. Hata hivyo taarifa hiyo haikutaja idadi hasa ya magaidi wa Boko Haram waliouawa kwenye operesheni hiyo.

Mashambulizi ya genge la ukufurishaji la Boko Haram yalianza miaka 10 iliyopita huko Nigeria na hadi sasa yameshapelekea watu wasiopungua 35 elfu kuuawa na zaidi ya milioni mbili wengine kuwa wakimbizi.

Magaidi wa Boko Haram wanafanya jinai kubwa magharibi mwa Afrika

 

Mashambulizi ya karibuni kabisa ya genge hilo ni yale yaliyotokea juzi na jana, baada ya wanamgambo wa Boko Haram kuvamia vijiji viwili katikati ya jimbo la Borno na kuua wakulima wanane. Wanne kati ya wakulima hao waliuawa kwa kuchinjwa na kukatwa vichwa na magaidi hao.

Mashambulio ya wanamgambo wa Boko Haram yameenea katika nchi nne zinazopakana na Ziwa Chad za Nigeria, Cameroon, Niger na Chad. 

Tags