Rambirambi zaendelea kutolewa kufuatia kifo cha Robert Mugabe
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55844-rambirambi_zaendelea_kutolewa_kufuatia_kifo_cha_robert_mugabe
Viongozi mbalimbali wa dunia wameendelea kutuma salamu zao za ramabirambi kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe kilichotokea jana huko nchini Singapore.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 07, 2019 02:32 UTC
  • Rambirambi zaendelea kutolewa kufuatia kifo cha Robert Mugabe

Viongozi mbalimbali wa dunia wameendelea kutuma salamu zao za ramabirambi kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe kilichotokea jana huko nchini Singapore.

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema katika salamu zake za rambirambi kwamba, amepokea kwa masikitiko habari ya kifo cha Robert Mugabe na kubainisha kwamba, alikuwa kiongozi jasiri na shupavu.

Akitoa salamu zake za pole na ramabirambi kwa taifa la Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa, Mugabe alikuwa bingwa wa Afrika aliyesimama kidete kuendesha mapambano dhidi ya wakoloni.

Serikali ya China kupitia Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo imetoa mkono wa pole kwa taifa la Zimbabwe na  kueleza kwamba, Mugabe alikuwa kiongozi bora wa harakati za ukombozi.

Robert Mugabe alipokuwa matibabuni nchini Singapore

Aidha balozi mbalimbali za kigeni mjini Harare zimtuma salamu za rambirambi kwa serikali na taifa la Zimbabwe kufuatia kifo cha baba wa taifa hilo Robert Gabriel Mugabe.

Hata hivyo habari kutoka Zimbabwe zinasema kuwa, kifo cha Mugabe kimewagawa wananchi wa nchi hiyo katika makundi mawili ambapo kuna wanaomtaja kama shujaa na mkombozi huku kundi la pili likimuelezea kama dikteta na mkandamizaji.

Robert Mugabe ambaye aliiongoza Zimbabwe kwa karibu miongo minne tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa mkoloni Muingereza mwaka 1980, alilazimishwa kujiuzulu mwezi Novemba mwaka juzi baada ya mapinduzi ya jeshi.