Unicef: Mamilioni ya watoto wanasumbuliwa na utapiamlo
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa mamilioni ya watoto duniani wanasumbuliwa na utapiamlo.
Ripoti iliyotolewa na UNICEF imesema kuwa, nusu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kote duniani hawapati virutubishi na madini ya kutosha, suala ambalo linawasababishia matatizo kama ya kuona, kusikia na dosari katika mfumo wa kinga ya mwili.
UNICEF imesisitiza katika ripoti hiyo kwamba, ukosefu wa aina hii wa lishe unatambuliwa kuwa ni "njaa ya siri" (hidden hunger).
Ripoti hiyo imesema kuwa, thuluthi moja ya jamii ya watoto milioni 700 wenye umri wa chini ya miaka mitano duniani wanasumbuliwa na utapiamlo.
kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNICEF pia inakadiriwa kwamba, zaidi ya watu milioni 800 kote duniani wanasumbuliwa na utapiamlo.