Magaidi sita waangamizwa katika operesheni iliyofanywa na jeshi nchini Burkina Faso
(last modified Sun, 01 Dec 2019 03:07:17 GMT )
Dec 01, 2019 03:07 UTC
  •  Magaidi sita waangamizwa katika operesheni iliyofanywa na jeshi nchini Burkina Faso

Jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa magaidi sita wameuliwa katika operesheni iliyofanywa na askari wa jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imeeleza kuwa, wanachama wa kundi moja la kigaidi pamoja na kiongozi wa kundi hilo aitwaye Abdulhadi wameuliwa katika operesheni iliyofanywa na vikosi vya jeshi hilo.

Aidha, jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa, askari wa jeshi la nchi hiyo wamenasa ghala kubwa la silaha.

Askari wa jeshi la Burkina Faso

Inasemekana kuwa, kiongozi huyo wa genge hilo la kigaidi amechangia kufanikisha kuundwa kundi la kigaidi liitwalo Ansarul-Islam katika eneo hilo la magharibi mwa Afrika.

Katika miezi ya karibuni, makundi ya kigaidi yamezidisha mashambulio yao nchini Burkina Faso na kuwafanya watu nusu milioni walazimike kuyahama makazi yao katika eneo hilo.

Magaidi wa kundi linalojiita Ansarul-Islam katika eneo la Afrika Magharibi wana mfungamano kifikra na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Daesh.

Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, mamia ya watu wameuliwa nchini Burkina Faso katika hujuma na mashambulio ya utumiaji silaha yaliyofanywa na makundi ya kigaidi.../