Wahajiri 40 wafariki dunia baada ya boti yao kughariki pwani mwa Mauritania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62664-wahajiri_40_wafariki_dunia_baada_ya_boti_yao_kughariki_pwani_mwa_mauritania
Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, wahajiri 40 wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kughariki katika maji ya pwani mwa Mauritania.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 07, 2020 02:16 UTC
  • Wahajiri 40 wafariki dunia baada ya boti yao kughariki pwani mwa Mauritania

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, wahajiri 40 wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kughariki katika maji ya pwani mwa Mauritania.

Vincent Cochetel ambaye ni afisa wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa ameasema kuwa, ajali hiyo imetokea katika pwani ya eneo la Nouadhibou na kwamba abiria 40 wa boti hiyo wamefariki dunia na mmoja tu ndiye aliyeokoka. 

Cochetel ameongeza kuwa, UNHCR, Shirika la Wahajiri la Umoja wa Mataifa (IOM) na maafisa wa serikali ya Mauritania wanafanya jitihada za kuzuia kukariri matukio kama haya lakini juhudi hizo zinakwamishwa na makundi ya wafanya magendo.

Ripoti zinasema wahajiri hao walitokea Morocco na walikuwa njiani kuelekea Uhispania. 

Wahajiri

Mgogoro mkubwa wa wahajiri unaozizonga nchi za Ulaya umesababishwa na sera mbaya za nchi za Magharibi katika maeneo mbalimbali hususa katika eneo la magharibi mwa Asia na vilevile umaskini mkubwa na ukosefu wa usalama katika baadhi ya nchi za Afrika.