Feb 17, 2021 02:27 UTC
  • Waliofariki kutokana na Ebola Guinea wafika 15

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Guinea sasa imeongezeka na kufikia watu watano huku waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo hatai wakiwa ni 15.

Kwa mujibu wa takwimu za mashirika ya afya ya Guniea, watu zaidi ya 150 walikuwa karibu na watu waliothibitishwa, wakiwemo 115 katika mkoa wa Enzeleikelei, na wengine 10 kwenye mji mkuu Conakry, ambapo asilimia 95 ya watu waliokuwa karibu na wagonjwa waliothibitishwa wamewekwa chini ya uangalizi wa kimatibabu.

Siku ya Jumamosi, Guinea ilitangaza maambukizi mapya ya Ebola, hii ikiwa ni mara ya kwanza ugonjwa huo kuripotiwa nchini humo tokea ule mlipuko wa Afrika Magharibi wa mwaka 2013-2016 ambao ulipelekea watu zaidi ya 11,300 kupoteza maisha Guinea, Liberia, na Sierra Leone.

Rais George Weah

Waziri Mkuu  Ibrahima Kassory Fofana amesema Guinea imeweka mkakati maalumu wa kukabiliana na Ebola hivyo amewataka wananchi wasiwe na wasiwasi na wafuate maagizo ya kiafya. 

Katika nchi jirani ya Liberia, Rais George Weah ametangaza hali ya dharura na kuziweka mamlaka za afya za nchi hiyo katika kiwango cha juu cha tahadhari baada ya vifo vinavyotokana na Ebola kuripotiwa nchini Guinea.

Rais  Weah ameamuru mamlaka za afya za nchi hiyo kuongeza ufuatiliaji wa karibu wa hali inayoendelea pamoja na kuchukua hatua za udhibiti kufuatia ripoti ya kuzuka homa ya Ebola katika nchi jirani ya Guinea.

Tags