Vijana wa Afrika Mashariki washiriki Mashindani ya Kimataifa ya Qurani ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7075-vijana_wa_afrika_mashariki_washiriki_mashindani_ya_kimataifa_ya_qurani_ya_iran
Vijana kutoka kanda ya Afrika Mashariki ni miongoni mahuffadh na maqari wanaoshiriki duru ya 33 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani inayofanyika hapa mjini Tehran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2016 10:24 UTC

Vijana kutoka kanda ya Afrika Mashariki ni miongoni mahuffadh na maqari wanaoshiriki duru ya 33 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani inayofanyika hapa mjini Tehran.

Mashindano hayo yalianza rasmi siku ya Jumatano katika Ukumbi Mkubwa wa Swala wa Imam Khomeini MA na yanatazamiwa kuendelea hadi Mei 17. Sheikh Ali Mohammadi, Mwakilishi wa Faqihi Mtawala na Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran amesema kuna washiriki 130 kutoka nchi 75 duniani ambao wanashiriki katika mashindano hayo ya kila mwaka.  Radio Tehran imepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wa kanda ya Afrika Mashariki wanaoshiriki mashindano hayo………