Marais wa Malawi na Mauritania wamtumia Raeisi salamu za pongezi
(last modified Thu, 01 Jul 2021 03:26:48 GMT )
Jul 01, 2021 03:26 UTC
  • Marais wa Malawi na Mauritania wamtumia Raeisi salamu za pongezi

Marais wa nchi za Afrika za Malawi na Mauritania wamemtumia ujumbe Rais mteule wa Iran, Hujjatul Islam Walmuslimin Ebrahim Raeisi wakimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi amemtumia ujumbe Ayatullah Sayyid Ebrahim Raeisi kwa kupata ushindi katika uchaguzi wa Rais uliofanyika Juni 18.

Sanjari na kulitakia kheri na fanaka taifa la Iran, Rais Chakwera amesisitizia haja ya kuimarishwa ushirikiano kati ya nchi yake na Iran kwa maslahi ya amani na usalama wa dunia.

Wakati huo huo, Rais Mohammed Bin Sheikh Al-Ghazwani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania mbali na kumpongeza Raiesi kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi huo, lakini ametilia mkazo juu ya umuhimu wa kuimarishwa uhusiano wa pande mbili.

Rais wa Malawi

Amegusia juu ya utayarifu wake wa kufanya jitihada za kunyanyua zaidi uhusiano wa kidugu na kirafiki wa nchi mbili hizi za Kiislamu kwa maslahi ya wananchi wa nchi hizi.

Viongozi wengine wa nchi za Afrika waliotumia salamu za pongeza Sayyid Raeisi kwa ushindi wake katika Uchaguzi wa Rais wa mwezi uliopita wa Juni ni pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Muhammadu Buhari wa Nigeria.

Sayyid Ebrahem Raeisi alitangazwa mshindi katika kinyang'anyiro hicho cha Juni 18 mwaka huu, kwa kupata kura karibu milioni 18 za wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu.