Watu 10 wauawa msikitini katika hujuma ya kigaidi Niger
(last modified Thu, 14 Oct 2021 06:04:16 GMT )
Oct 14, 2021 06:04 UTC
  • Watu 10 wauawa msikitini katika hujuma ya kigaidi Niger

Taarifa zinasema kuwa watu 10 wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililolenga msikiti wa kijiji kimoja huko magharibi mwa Niger.

Vyombo vya habari nchini Niger vimeripoti kuwa Waislamu hao 10 waliuawa katika hujuma iliyolenga msikiti wa kijiji cha cha eneo la Tillabéri huko magharibi mwa Niger.

Afisa wa serikali ya Niamey katika mji wa Banibangou ambao ni makao makuu ya eneo la Tillabéri amethibitisha kuwa, watu 10 wameuawa katika hujuma hiyo ya kigaidi. 

Ripoti hiyo inasema kuwa hadi sasa watu zaidi ya 450 wameuawa katika mashambulizi ya kigaidi huko magharibi mwa Niger tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2021.

Hivi karibuni wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliripoti kuwa, katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2021 Afrika ndiyo iliyokumbwa na madhara makubwa zaidi kutokana na harakati za makundi ya kigaidi kama Daesh na al Qaida.

Wataalamu hao wanasema kuwa, kupanuka harakati za makundi hayo ya kigaidi katika baadhi ya nchi za Afrika kama Mali, Burkina Faso, Ivory Coast, Senegal, Somalia, Niger, Cameroon, Nigeria, Chad, Kenya, Msumbiji na Tanzania kunatia wasiwasi.

Tags