May 27, 2016 15:27 UTC
  • Watu wanane wauawa katika shambulizi msikitini Sudan

Watu wanane wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa msikitini na watu waliokuwa na silaha katika mji wa al Junaynah mkoani Darfur Magharibi huko Sudan.

Shirika la habari la kimataifa la Qurani (Iqna) limeripoti leo kuwa shambulizi hilo lililofanywa na kundi la watu wenye silaha katika eneo la Azaran karibu na mji wa al Junaynah limetajwa kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi.

Kufuatia shambulio hilo, maafisa husika wa mkoa wa Darfur wamezidisha idadi ya wanajeshi kutokana na kuweko uwezekano wa kufanyika maandamano ya wananchi na kusababisha ghasia mitaani.

Hii ni katika hali ambayo mizozo ya kikabila katika mji wa al Junaynah imesababisha hali ya wasiwasi miongoni mwa wakazi wa mji huo na viongozi wa mji huo huko Darfur Magharibi. Hadi kufikia sasa jitihada rasmi za kumaliza mizozo hiyo ya kikabila zimegonga mwamba na inasemekana kuwa hali hiyo imekuwa na taathira hasi kwa muundo wa kijamii wa mji huo. Aidha kuongeza ghasia na mashambulizi chungu nzima katika mji wa al Junaynah kunasababishwa na mambo mengi tu moja ikiwa ni kukosekana udhibiti na usimamizi mzuri wa hali ya usalama na makundi yanayobeba silaha, masuala yanayorahisisha upatikanaji silaha kwa makabila yanayozozana.

Tags