Jun 08, 2016 06:53 UTC
  • Serikali ya Nigeria: Tupo tayari kuzungumza na waasi wa Niger Delta

Hatimaye serikali ya Nigeria imewaalika waasi wa Ulipizaji Kisasi wa Niger Delta kwa ajili ya mazungumzo ya kuhitimisha mgogoro wa kusini mwa nchi hiyo.

Emmanuel Ibe Kachikwu, mwakilishi wa serikali ya Nigeria katika sekta ya mafuta ametangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo imeazimia kufanya mazungumzo ya amani na waasi wa Niger Delta ili kurejesha usalama kusini mwa taifa hilo. Amesema, Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria tayari amelitaka jeshi kusimamisha operesheni zake za wiki mbili katika eneo hilo ili kuwezesha viongozi wa serikali na wale wa waasi kufanya mazungumzo ya kupatiwa ufumbuzi mgogoro uliopo. Emmanuel Ibe Kachikwu amesisitiza kuwa, serikali imeazimia kuhakikisha amani ya kweli inarejea katika eneo la Delta, hasa kwa kuwa harakati za Ulipizaji Kisasi za waasi hao zimeathiri pakubwa uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria. Hii ni katika hali ambayo jeshi la nchi hiyo limetuma meli na ndege za kijeshi katika eneo la Niger Delta kwa ajili ya kukabiliana na waasi hao.

Tags