Waasi 40 wa Burundi wauawa mashariki mwa Kongo DR
(last modified Mon, 28 Nov 2022 07:16:09 GMT )
Nov 28, 2022 07:16 UTC
  • Waasi 40 wa Burundi wauawa mashariki mwa Kongo DR

Makumi ya waasi raia wa Burundi wameuawa katika operesheni ya pamoja ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi mashariki mwa DRC.

Hayo yalisemwa jana na Luteni Marc Elongo-Kyondwa, Msemaji wa Jeshi la Kong DR na kufafanua kuwa, wapiganaji 40 wa Kirundi wa kundi la waasi la National Liberation Forces (FNL) wameuawa katika operesheni ya askari wa DRC wakishirikiana na wenzao wa Burundi.

Amesema majeshi ya DRC na Burundi yamewashambuliwa waasi wa FNL kutoka milima minne inayouzunguka mji wa Nabombi, ambapo 40 miongoni mwao wamengamizwa.

FNL ni tawi la kundi la zamani la waasi lililokuwa likiongozwa na Agathon Rwasa, ambaye kwa sasa ni kinara wa upinzani nchini Burundi.

Hii ni katika hali ambayo, mkutano wa viongozi kuhusu amani na usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliofanyika Luanda Angola tarehe 23 mwezi huu wa Novemba ulisema kuwa, pande husika kwenye mapigano mashariki mwa DRC zimeafikiana kusitisha vita.

Mapigano yalivyopelekea wakazi wa mashariki mwa DRC kuyakimbia makazi yao

Mapigano, harakati za magenge ya waasi na utovu wa usalama mashariki mwa DRC vimeimazimisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuingilia kati ili kujaribu kurejesha utulivu katika eneo hilo. Ingawa mazungumzo yalikuwa kipaumbele lakini EAC ilituma kikosi chake mashariki mwa DRC ili kuwashinikiza waasi wa M23 na megenge mengine ya wabeba silaha.

Askari wa Burundi wapo katika eneo la Kivu Kusini nchini DRC tangu Agosti mwaka huu, kama sehemu ya kikosi hicho cha pamoja cha EAC. Kenya imeshatuma mamia ya askari wake nchini humo, huku Uganda ikitazamiwa kutuma wanajeshi wake mwishoni mwa mwezi huu.

Tags