Morocco na Ufaransa kupepetana nusu faina ya Kombe la Dunia
Timu za soka za taifa za Ufaransa na Morocco zitakutana katika hatua ya nuusu ya fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea huko nchini Qatar.
Mchuano huo kati ya mabingwa watetezi Ufaransa na mwakilishi pekee wa Afrika unatarajiwa kuwa wa aina yake hasa kwa kutilia maanani kiwango cha soka kilichoonyesghwa hadi sasa na Morocco. Morocco ambayo imeandika historia kwa kuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kutinga nusu fainali imepania kufanya maajabu na kuvuruga tabiri zote zilizoelezwa kabla ya kuanza mashindano hayo.
Morocco itakutana na Ufaransa baada ya kupeleka habari ya msiba nchini Ureno pale ilipofuta ndoto za Ronaldo na wenzake za kusonga mbele katika mashindano hayo.
Bao la ushindi la Morocco lilifungwa dakika za mwisho za kipindi cha kwanza wakati Youssef En-Nesyri alipoteleza na kushinda kwa kichwa krosi iliyopigwa na Yahya Attiat-Allah. Kipa wa Portugal Diogo Costa alijaribu kumzuia En-Nesyri kwa krosi lakini En-Nesyri alimruka kila mmoja na kuutumbukiza mpira wavuni.
Timu ya taifa ya soka ya Ufaransa kwa upande wake imejikatia tiketi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Uingereza bao 2-1 katika uwanja wa Al Thumama.
Iliwachukua Ufaransa dakika 17 tu kupata bao lao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Aurelien Tchouameni.
Na Uingereza waliendelea kupambana na katika dakika ya ..ya kipindi chab pili walifanikiwa kupata penati na Harry Kane alisawazisha katika dakika ya 54.
Ufaransa waliendelea na mashabulizi na kujipatia bao la pili katika dakika ya 78 mpira wa kichwa uliopigwa na Olivier Giroud ulikwenda moja kwa moja na kutinga wavuni kutokana na makosa yaliofanywa na Harry Maguire.
Uingereza itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikosa penalti ambayo wangeweza kusawazisha baada ya Harry Kane kupiga juu mpira huo na kutoa mpira nje.