Mashambulio ya kikatili ya Marekani yaongezeka nchini Somalia
(last modified Tue, 10 Jan 2023 02:34:41 GMT )
Jan 10, 2023 02:34 UTC
  • Mashambulio ya kikatili ya Marekani yaongezeka nchini Somalia

Tovuti moja ya nchini Marekani imetangaza habari ya kuongezeka mashambulizi ya anga ya Marekani nchini Somalia wakati wa urais wa "Joe Biden" na mauaji ya raia katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Marekani imekuwa ikifanya kile kinachodaiwa ni oparesheni za anga za eti kupambana na ugaidi nchini Somalia kwa muda mrefu sasa.

Africom, komandi ya kijeshi ya Marekani barani Afrika, imekiri mara kadhaa kwamba imekuwa ikiua raia katika operesheni za jeshi la Marekani nchini Somalia.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Fars, jana Jumatatu, tovuti ya Military Times, ilinukuu ripoti ya Komandi ya Kijeshi ya Marekani Barani Afrika (AFRICAM), ikisema kwamba jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi zaidi ya 12 ya anga nchini Somalia mwaka 2022, na hilo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 30 ya mashambulio ya Marekani huko Somalia ikilinganishwa na mwaka jana.

 

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, baadhi ya Wabunge wa Marekani wamekagua operesheni ya Africom na wanaamini kuwa hakutolewi idadi sahihi ya raia wanaokuwa wahanga wa mashambulio hayo ya Marekani.

Baadhi ya wabunge wa Baraza la Congress wamenaamini kuwa operesheni zinazodaiwa ni za kupambana na ugaidi za Pentagon barani Afrika na hasa nchini Somalia kuwa hazifanywi inavyotakiwa na kusisitiza kuwa, raia wa kawaida ni wahanga wakuu wa mashambulizi hayo ya anga ya Marekani.

Tags