Waafrika wamwambia Makamu wa Rais wa Marekani: Hatutaki ushoga
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i95704-waafrika_wamwambia_makamu_wa_rais_wa_marekani_hatutaki_ushoga
Ziara inayofanywa na Makamu wa Rais wa Marekani katika nchi tatu za Afrika imeambatana na malalamiko na wasiwasi mkubwa baina ya raia wa nchi za Afrika ambao wanamini kuwa moja ya malengo muhimu ya kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Marekani barani Afrika ni kupigia debe ushoga na usagaji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 30, 2023 08:41 UTC
  • Waafrika wamwambia Makamu wa Rais wa Marekani: Hatutaki ushoga

Ziara inayofanywa na Makamu wa Rais wa Marekani katika nchi tatu za Afrika imeambatana na malalamiko na wasiwasi mkubwa baina ya raia wa nchi za Afrika ambao wanamini kuwa moja ya malengo muhimu ya kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Marekani barani Afrika ni kupigia debe ushoga na usagaji.

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris aliwasili nchini Tanzania jana usiku baada ya kukamilisha ziara yake nchini Ghana ambako alikosolewa vikali kutokana na matamshi yake ya kutetea vitendo vichafu vya maingiliano ya kingono baina ya watu wenye jinsia moja. Kamala Harris aliwaambia waandishi wa habari akiwa Ghana kwamba ushoga na vitendo vya maingiliano ya ngono kati watu wenye jinsia moja ni miongoni mwa haki za binadamu!

Akijibu matamshi hayo, Spika wa Bunge la Ghana amemkosoa vikali Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, kutokana matamshi yake kuhusu haki za watu wanajihusisha na ushoga na maingiliano ya kujamiiana baina ya watu wa jinsia moja nchini Ghana.

Spika Alban Bagbin ameyataja matamshi ya Kamala Harris kuhusu kundi hilo kuwa "si ya kidemokrasia."

“Kamala Harris anafanya nini? Hatuwezi kuvumilia mambo hayo na si ya kidemokrasia… hatutamvumilia mtu anayekuja kutueleza nini kizuri na kipi kibaya?”, amesema Spika wa Bunge la Ghana akikosoa matamshi ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Haris aliyetetea ubaradhuli akiutaja kuwa ni haki ya binadamu.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, Wabunge wa Ghana wamependekeza kifungo cha miaka 10 jela ndani ya muswada mpya ambao unaharamisha vitendo vya ushoga na usagaji.

Baada ya safari yake nchini Tanzania, Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ataelekea Zambia ambako tayari vyama vya upinzani vimepanga kufanya maandamano sambamba na safari hiyo kupinga ushoga na ubaradhuli.

Kamala Harris

Wabunge 50 wa upinzani wanasema safari ya Kamala Harris nchini humo ni sehemu ya ajenda ya kulazimisha haki za mashoga na wasagaji kwa Wazambia.

Mapema mwezi huu Rais wa Zambia Bw Hakainde Hichilema aliahidi kuunga mkono sheria ambazo zinaharamisha ushoga.

Huku Tanzania siku chache zilizopita Dk. Harrison Mwakyembe aliyewahi kuongoza wizara kadhaa katika serikali ya nchi hiyo ikiwemo Wiziri ya Mambo ya Katiba na Sheria aliunga mkono msimamo wa Rais Suluhu Hassan na Makamu wake, Philip Mpango wa nchi hiyo wa kupinga ushoga na usagaji: