Uhaba wa chakula watishia maisha ya mamilioni ya watu barani Afrika
Takriban watu milioni 20 katika Pembe ya Afrika wanakabiliwa na viwango vya kutisha vya uhaba wa chakula.
Nchi za Pembe ya Afrika zinakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo katika kipindi cha takriban miaka 70 iliyopita, kutokana na mvua ya kutosha kutonyesha kwa misimu sita mfululizo.
Zaidi ya watu milioni 20 katika eneo hilo kwa sasa wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula. Mafuriko ya ghafla na yasiyotarajiwa yameikumba Somalia hivi karibuni na kufanya mgogoro wa chakula katika nchi hiyo kuwa mbaya zaidi. Nchi kadhaa za Afrika Mashariki karibuni zimewekwa katika orodha ya Umoja wa Mataifa inayoitwa "Maeneo yenye migogoro ya njaa".
Mwaka huu, karibu watu milioni 43 wanakabiliwa na uhaba wa chakula Afrika Magharibi, mara nne zaidi ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani karibuni lilionya kwamba mzozo wa njaa katika Pembe ya Afrika unatishia maisha ya mamilioni ya watu katika eneo hilo. Baada ya miaka 3 ya ukame, zaidi ya watu milioni 23 wanakabiliwa na njaa kali katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema linahitaji msaada wa kifedha wa dola milioni 810 ili kukidhi mahitaji ya dharura.
Katika ripoti yake ya hivi karibuni, shirika hilo lilitahadharisha kwamba mamilioni ya watu katika Pembe ya Afrika wanakabiliwa na hali ya dharura ya njaa, huku eneo hilo likitumbukia kutoka kwenye janga moja hadi jingine. Ukame wa muda mrefu zaidi kuwahi kusajiliwa katika eneo hilo umeibuka kuwa mgogoro tofauti wa mvua kubwa na mafuriko.
Nchini Kenya, serikali inatoa chakula kwa watoto 2,000 kila siku na kuwapa fursa ya masomo.
Wakati huo huo, mafuriko katika mji wa Western Cape nchini Afrika Kusini yamechukua maisha ya mtu mmoja.