-
Mkutano wa Rais wa Ufaransa na wanaoipinga Iran ni hatua ya kuchochea machafuko
Nov 14, 2022 04:31Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani kikao cha Rais wa Ufaransa na wapinzani wa Iran na kukitaja kitendo hicho kuwa ni ukiukaji mkubwa wa majukumu ya kimataifa ya Ufaransa katika kupambana na ugaidi na ukatili.
-
Kutumiwa siasa na Magharibi katika suala la haki za binadamu
Nov 13, 2022 22:52Mkuu wa Masuala ya Kimataifa ambaye pia na Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Idara ya Mahakama ya Iran amesema, inasikitisha kwamba leo hii haki za binadamu zinatumiwa zaidi kisiasa kuliko ilivyowahi kuwa wakati wowote ule.
-
Kilichofanyika Bahrain ni uchaguzi au uteuzi tu wa watu?
Nov 13, 2022 05:40Jana Jumamosi, ulifanyika uchaguzi nchini Bahrain wa kuchagua wabunge 40 wa Baraza la Wawakilishi na wajume 30 wa Mabaraza ya Miji.
-
Mashinikizo mapya ya Magharibi dhidi ya Iran baada ya kushindwa mradi wa kuibua ghasia
Nov 12, 2022 22:52Nchi za Magharibi baada ya kushindwa mradi wao wa kuibua ghasia nchini Iran sasa zinatafuta njia nyingine mpya mbadala ili kuiwekea mashinikizo Tehran. Katika uwanja huo, nchi za Magharibi khususan za Ulaya mbali na kuratibu vikwazo vipya zimejielekeza katika kutoa taarifa na maazimio dhidi ya Iran sambamba na kushadidisha mashinikizo ya kisiasa dhidi ya nchi hii.
-
Jitihada za kufunga kituo cha Kiislamu cha Hamburg, Ujerumani
Nov 12, 2022 08:48Katika juhudi za madola ya Magharibi za kuunga mkono ghasia na machafuko nchini Iran, vyama vya muungano unaotawala nchini Ujerumani vimetoa wito wa kufungwa Kituo cha Kiislamu na Kiutamduni cha Iran katika mji wa Hamburg nchini humo.
-
Mapambo ya uchaguzi wa Bahrain; demokrasia bandia ya ukoo wa Aal-Khalifa
Nov 11, 2022 22:59Katika hali ambayo uchaguzi wa bunge la Bahrain umaanza masaa machache yaliyopita, viongozi wa kisiasa na kidini wa nchi hiyo wametoa wito wa kususiwa uchaguzi huo.
-
Iran yasisitiza sera zake za kuwa na uhusiano na ujirani mwema na majirani zake.
Nov 11, 2022 03:19Nasser Kanaani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huku akijibu madai ya hivi karibuni ya Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan kuhusiana na eti uungaji mkono wa Iran kwa Armenia, amesisitiza kuwa sera kuu za Iran zimejengeka katika msingi wa kuwa na ujirani mwema na kupanua mahusiano na majirani wake wote na kuwa kuimarisha uhusiano na mmoja wa majirani hao hakuna maana ya kufanya uadui na majirani wengine.
-
Onyo la Iran kwa Uingereza kwa vitendo vyake vya kiharibifu humu nchini
Nov 10, 2022 23:36Waziri wa Usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika matukio ya hivi karibuni ya humu nchini, "mkono wa utawala wa Kizayuni katika utekelezaji, mkono wa Uingereza katika propaganda na mkono wa utawala wa kiimla wa Aal Saud katika kugharamia machafuko, imeonekana wazi zaidi."
-
Nguvu za Muqawama; sababu kuu ya kutiwa saini makubalino ya mipaka ya baharini
Nov 10, 2022 05:20Hivi karibuni, Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel zilitiliana saini makubaliano ya mpaka wa baharini kwa upatanishi wa Marekani. Hivi sasa lakini Benjamin Netanyahu anadai kuwa hatoheshimu makubaliao hayo.
-
Kuendelea mgogoro wa Sudan; kuongezeka uingiliaji wa kigeni na malalamiko ya wananchi
Nov 09, 2022 21:53Mgogoro wa Sudan umezidi kupanuka na kuchukua wigo mpana huku maandamano ya wananchi yakiendelea kushuhudiwa kila leo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.