Jul 28, 2023 07:46 UTC
  • Maombolezo ya Ashura ya Imamu Hussein AS yaanza kote nchini Iran

Maombolezo ya Ashura ya Bwana wa Mashahidi, Imamu Hussein AS yameanza kote nchini katika Iran ya Kiislamu.

Wananchi katika Iran ya Kiislamu, leo Ijumaa inayosadifiana na Ashura ya Imamu Hussein, wamemiminika mitaani katika miji yote nchini kushiriki kwenye maombolezo ya Jemedari na Bwana wa Mashahidi.
Vikundi vya waombolezaji vinamuomboleza Imamu Hussein AS na masahaba zake waaminifu kwa kusoma kasida za maombolezo na kujipiga vifua.
 
Leo Ijumaa, inayosadifiana na siku ya kumi ya mwezi wa Muharram 1445 Hijria ni siku ya Ashura ya Imamu Hussein AS.
Maombolezo ya Muharram nchini Iran

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran Press, Hadhrat Aba Abdillah Al-Hussein AS na masahaba zake waaminifu waliuawa shahidi huko Karbala mnamo tarehe 10 Muharram  mwaka 61 Hijria.

 
Licha ya kupita karne nyingi tangu lilipojiri tukio la kuunguliza na kusononesha nyoyo la Karbala na kuuawa shahidi Imamu Hussein AS na masahaba zake waaminifu, sio tu umuhimu na hadhi ya tukio hilo haijapungua, bali kadiri muda unavyosonga mbele, ujumbe wa Ashura unazidi kuenea na hafla za maombolezo zinafanyika kwa shauku na hamasa kubwa na uelewa mpana zaidi.../

 

Tags