Kan'ani: Wazayuni wanafanya jinai Gaza mbele ya macho ya walimwengu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i110130-kan'ani_wazayuni_wanafanya_jinai_gaza_mbele_ya_macho_ya_walimwengu
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema jinai za kutisha za kivita zinazofanywa na Wazayuni eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina zinaendelea mbele ya macho ya walimwengu.
(last modified 2024-03-31T23:52:29+00:00 )
Mar 31, 2024 23:52 UTC
  • Kan'ani: Wazayuni wanafanya jinai Gaza mbele ya macho ya walimwengu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema jinai za kutisha za kivita zinazofanywa na Wazayuni eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina zinaendelea mbele ya macho ya walimwengu.

Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba, shambulio dhidi ya mahema ya wakimbizi wa Kipalestina katika maeneo ya jirani na Hospitali ya Mashahidi ya Al-Aqsa huko Deir ul-Balah, ambayo yameua na kujeruhi idadi kubwa ya Wapalestina, ni jinai ya karibuni zaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoua watoto, ambao unakiuka sheria na kanuni zote za kimataifa.

Kan'ani ameongeza kuwa, jamii na taasisi za kimataifa zinataka kuzuiwa mara moja jinai hizo na kufunguliwa mashitaka dhidi ya wahalifu wa Kizayuni. 

Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameeleza kuwa, jinai za kinyama zinazofanywa na Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza ni doa la fedheha ya milele na lisilofutika katika mapaji ya nyuso za waungaji mkono wanafiki wa utawala huo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, tangu kuanza kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, Wapalestina 32,782, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, wameuawa shahidi na wengine 75,298 wamejeruhiwa.