Iran na Saudia zasisitiza kupanua na kustawisha uhusiano wao
(last modified Sat, 01 Jun 2024 02:21:59 GMT )
Jun 01, 2024 02:21 UTC
  • Iran na Saudia zasisitiza kupanua na kustawisha uhusiano wao

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia wamesisitiza kustawishwa uhusiano wa pande mbili katika mazungumzo waliyofanya kwa njia ya simu.

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limeripoti kuwa Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza katika ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuhusu mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan na kufafanua kwamba: "kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi mbili tuna uhakika kwamba wafanyaziara wa Iran watatekeleza ibada ya Hija katika mazingira ya usalama na utulivu".

Katika mazungumzo hayo aliyofanya na Faisal bin Farhan, Bagheri ameishukuru Saudi Arabia kwa hatua ya maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo ya kuhudhuria mazishi ya Shahidi Rais Seyyed Ebrahim Raisi na Shahidi Hossein Amir- Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran.

 
Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuhusu waliyojadili na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia katika mazungumzo hayo waliyofanya kwa njia ya simu ya kwamba: "mbali na kuiangazia hali mbaya ya sasa ya mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Ghaza na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni, tumesisitizia kuchukua hatua madhubuti na za pamoja ili kuzuia kuendelea mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo ghasibu../

 

Tags