'Fikra za Imam Khomeini bado zinahamasisha harakati za ukombozi duniani'
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i112488-'fikra_za_imam_khomeini_bado_zinahamasisha_harakati_za_ukombozi_duniani'
Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema itikadi za hayati Imam Khomeini, Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, bado zinatia msukumo harakati za ukombozi kote duniani.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jun 02, 2024 23:25 UTC
  • 'Fikra za Imam Khomeini bado zinahamasisha harakati za ukombozi duniani'

Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema itikadi za hayati Imam Khomeini, Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, bado zinatia msukumo harakati za ukombozi kote duniani.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, kamandi hiyo imesema kuwa fikra za Imam Khomeini ya kusimama dhidi ya ubeberu imefika katika pembe za mbali za dunia, na kupelekea mabadiliko katika mahesabu na mipango ya madola makubwa duniani.

Taarifa hiyo imetolewa katika mkesha wa kumbukumbu ya kuaga dunia Imam Khomeini, kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979 ambaye aliongoza  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 tarehe 3 Juni 1989.

Imamu Khomeini (MA), muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 

Mamia ya maelfu ya watu hukusanyika katika kaburi lake kusini mwa Tehran kila mwaka kuadhimisha kumbukumbu hiyo na kutoa heshima kwa shakhsia huyu mashuhuri ambaye itikadi zake za kimapinduzi na harakati zake dhidi ya mfalme wa zamani wa Iran, Shah Pahlavi, ziliibua maporomoko ya kisiasa katika eneo hilo na duniani kote.

Fatwa ya Imam Khomeini kwa Waislamu ya kuwapiga marufuku kujihusisha na uhusiano wowote wa kisiasa au kibiashara na utawala wa Kizayuni wa Israel imekuwa mada kuu ya mjadala siku hizi, hususan katika nchi za Magharibi ambako hasira ya umma inazidi kupamba moto kuhusu hujuma inayoendelea ya Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.