Jun 21, 2024 13:11 UTC
  • Sayyid Abu Turabi Fard: Kushiriki katika uchaguzi kuna mchango katika kuongeza nguvu ya taifa

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa, kushiriki katika uchaguzi kuna mchango katika kuainisha hatima ya kuongeza nguvu ya taifa.

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mohammad Hossein Abu Turabi Fard kuwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi na kumchagua mtu anatestahiki zaiidi miongoni mwa wagombea kwa ajiili ya kuongoza serikali ni jambo lenye mchango muhimu katika kuongezeka nguvu na mamlaka ya taifa.

Sayyid Abu Turabi Fard amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa na kueleza kwamba, mfumo salama wa kisiasa unafungua njia ya jamii kupata maendeleo.

Akiashiria uchaguzi wa Rais hapa Iran utakaofanyika Ijumaa ijayo, Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Teran amesema kuwa, katika kipindi chote cha miongo minne iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iimekuwa na faili zuri na la kujifakharisha kuhusiana na uchaguzi kutokana na kuendesha chaguzi salama na katika mazingira huru na ya haki.

 

Kuhusiana na umuhimu uchaguzi, Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema, kama uchaguzi hautakuweko katika nchi, kutakuweko utawala wa kidikteta au kutakuwa na shaghalabaghala.

Abu Turabi Fardi amewaasa wapiga kura nchini Iran kuhakikisha kwamba, Ijumaa ijayo wanamchagua mtu anayestahiki zaidi miongoni mwa wagombea ili kushika wadhifa wa Rais kwa ajili ya kufanikisha malengo matukufu ya Mapinduzi, thamani za Kiislamu na ambaye ataleta maendeleo na ustawi wa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.