Helikopta ya walinda amani wa Umoja wa Afrika yaanguka Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i127864-helikopta_ya_walinda_amani_wa_umoja_wa_afrika_yaanguka_somalia
Helikopta ya Kikosi cha Usaidizi na Uimarishaji Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AUSOM) imeanguka leo Jumatano katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.
(last modified 2025-07-02T08:38:15+00:00 )
Jul 02, 2025 08:38 UTC
  • Helikopta ya walinda amani wa Umoja wa Afrika yaanguka Somalia

Helikopta ya Kikosi cha Usaidizi na Uimarishaji Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AUSOM) imeanguka leo Jumatano katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Afisa mmoja wa usafiri wa anga mjini Mogadishu, ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutokana na vikwazo vya kuzungumza na vyombo vya habari, amesema kuwa helikopta hiyo ya walinda amani ilikuwa imebeba watu wanane na ilianguka wakati wa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde, baada ya kuondoka katika kambi ya anga ya Balidoogle.

Afisa huyo amesema kuwa kuna majeruhi katika ajali hiyo, ingawa hakutaja idadi kamili ya waliojeruhiwa au waliopoteza maisha. Ameongeza kuwa vikosi vya uokoaji na zimamoto walifika eneo la tukio kwa haraka na wakafanikiwa kuzima moto uliotokea kwenye helikopta hiyo.

Ajali hiyo imesababisha ucheleweshwaji wa baadhi ya safari za ndege, lakini kwa mujibu wa taarifa za awali, shughuli katika uwanja wa ndege zimeanza kurejea katika hali ya kawaida.